'Mchukueni pia yeye,'Nyota Ndogo asema huku akimtambulisha mpenzi wake mitandaoni

Muhtasari
  • Nyota Ndogo amtambulisha mpenzi wake mitandaoni
  • Awali msanii huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikuwa amesema kwamba amekubali kuachwa na hatolia tena
  • Hii ni baada ya Nyota Ndogo kukosana na mumewe mzungu miezi chache iliyopita
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n

Msanii kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo amemtambulisha menzi wake mpya mitandaoni,na kufichua kwamba amempeleka kwa wazazi.

Awali msanii huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikuwa amesema kwamba amekubali kuachwa na hatolia tena.

Hii ni baada ya Nyota Ndogo kukosana na mumewe mzungu miezi chache iliyopita.

"Maumivu yameisha hakuna tena kulia. NIMERUDI NYUMBANI. SITOKI MILELE UKIWACHWA ACHIKA NIMEACHIKA,"Nyota Ndogo aliandika.

Aidha amesema kwamba ni wiki tatu sasa zimepita baada ya kupelekwa kwa wazazi na mpenzi wake Hurricane ambaye pia ni mwanamuziki.

Pia alimshukuru kwa kumpenda jinsi alivyo.

"So wiki Tatu zimepita toka aliponipeleka home kwa wazazi. Nilimwambia kama umeambia wazazi na kijiji unatka kumuoa nyota ndogo lazima niende bila makeup wanikubali nilivyo. @officialpday_hurrikane hakusita siamenikubali nilivyo japo wazazi walikustuka wakisema no huyu huyu WA watu na viatu akasema yes

Nikaimbishwa tulichinjiwa mbuzi hapo supu kwa wingi. Yenyewe umri unakwenda tunasubiri nini? @officialpday_hurrikane ahsante kwa kunipenda kama nilivyo. Haya nimemtag mchukueni pia yeye."

Kulingana na asiliia kubwa ya wanamitandao, wamedai kwamba ni wimbo ambao Nyota na mpenzi wake wanaandaa.

Je kulingana na maoni yako ni wimbo au ni mapenzi ya ukweli?