Anne Waiguru azungumza baada ya kuwa miongoni mwa wanawake wenye ushawishi mkubwa Afrika

Muhtasari
  • Anne Waiguru azungumza baada ya kuwa miongoni mwa wanawake wenye ushawishi mkubwa Afrika
  • Aidha alisema kwamba ni heshima kubwa  kuteuliwa kama mwanamke mwenye ushawaishi mkubwa Afrika
Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi
Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi
Image: MAKTABA

Gavana wa kaunti ya KIrinyaga Anne Waiguru hatimaye amevunja kimya chake baada ya katika orodha ya wanawake wenye ushawishi mkubwa Afrika nzima.

Waiguru pia aliwapongeza baadhi ya wanawake waliokwenye orodha hiyo ikiwemo Gavana wa Kitui Charity Ngilu, jaji mkuu Martha Koomr.

Aidha alisema kwamba ni heshima kubwa  kuteuliwa kama mwanamke mwenye ushawaishi mkubwa Afrika.

Miongoni mwa wanawake hao ni pamoja na,rais wa Tanzania Samia Suluhu,Ellen Johnson, Ngozi Okonjo-Iweala,Kaluki Ngilu,Sahle-Work Zewde,Renee Ngamau miongoni mwa wanawake wengine.

Cheo hicho kimewekwa na vyombo vya habari vya Avance, uhusiano wa umma na kampuni ya ukadiriaji.

Waiguru alibahatika kupata kutambuliwa kati ya wanawake waliosifiwa kwa kupanda ngazi ya ushirika, kuanzisha biashara zao wenyewe, au wamekuwa mstari wa mbele katika kufanya maamuzi katika mikutano yao na kwingineko.

" Heshima kuteuliwa kama mmoja wa Wanawake 100 wa Kiafrika wenye Ushawishi mkubwa wa Kiafrika -2021

Kushiriki nafasi na wanawake wazuri wa Afrika kama HE. Kituo cha Rais cha Wanawake na Maendeleo cha Ellen Johnson Sirleaf, H.E @ Sahle-Work Zewde, Ngozi Okonjo-Iweala, Chimamanda Ngozi Adichie, ananihimiza niendelee kuwasha moto kwa ujasiri

Hongera Mheshimiwa Charity Kaluki Ngilu, Jaji wa Kike Martha Koome, Renee Ngamau, na wanawake wengine waliofanya orodha hiyo," Aliandika Waiguru.