'Tuheshimu uchaguzi wa mtu,'Msanii Juliani na Lilian wawatumia wakosoaji wao ujumbe

Muhtasari
  • Msanii Juliani awatumia wakosoaji wake ujumbe
Image: INSTAGRAM// LILIAN NG'ANG'A

Baada ya Mwanamuziki Julius Owino almaarufu kama Juliani kujitokeza na kuzungumzia madai kuwa anachumbia aliyekuwa mke wa gavana Alfred Mutua Bi Lilian Ng'ang'a, alipokea vitisho ambavyo vilimbidi aende kuripoti kwa polisi.

Tangu Mutua na Lilian watangaze kuvunjika kwa ndoa yao mwezi uliopita uvumi  umekuwa ukitanda mitandaoni kuwa msanii huyo ndiye sababu kuu ya kutengana kwao.

Picha kadhaa  za msanii huyo akijivinjari na Lilian zimekuwa zikienezwa mitandaoni na kusemekana kuwa wamejitosa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, msanii huyo alichapisha ujumbe wa kimafumbo na kusema kuwa watu wana uhuru wa kufikiria wanavyotaka.

Ni wazi kuwa wawili hao ni wapenzi kwani kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewatumia wakosoaji wao ujumbe na kuwaambia kwamba wanapaswa kuheshimu uamuzi wa mtu.

"Picha hii ni watu wazima wazima wawili ambao wamechagua kuwa pamoja, hadithi nyingine yoyote ni ya kizamani na imepotea zamani na watu wenye nia mbaya wacha tuheshimu uchaguzi wa mtu, tupendane," Aliandika Juliani.

Wakati huo huo kupitia kwenye ukurasa wake Lilian pia alipakia picha yenye ujumbe ambao ulikuwa umeandikwa au kupakiwa na mpenzi wake Juliani.