'Ni ngumu lakini nitajaribu,'Mama yake Sharon Otieno kuwania kiti cha MCA mwaka ujao

Muhtasari
  • Leo ni miaka tatu tangu mwanafunzi wa Chuo Kikuu Sharon Otieno na mtoto wake ambaye hakuwa amezaliwa kuuwawa kinyama
sharon.otieno.
sharon.otieno.

Leo ni miaka tatu tangu mwanafunzi wa Chuo Kikuu Sharon Otieno na mtoto wake ambaye hakuwa amezaliwa kuuwawa kinyama.

Kulingana na duru za habari na taarifa kutoka mpasho Mama wa marehemu Sharon Otieno anatazamia kuwania  kiti cha MCA katika Kaunti ya Homabay.

Kulingana na Melida Auma, ameazimia kuwakilisha wadi ya Homa Bay Town Magharibi na pia kutafuta njia ya kuwatunza watoto wake na wajukuu ambao Sharon aliacha.

"Niliamua kujaribu kuwania kiti cha MCA kwa sababu ninataka maisha bora kwa watoto wangu na wajukuu. Ni ngumu, lakini nitajaribu," Auma aliambia Nation.

Kulingana na Auma, watu wengi walikuwa karibu na familia yake baada ya mauaji ya Sharon, lakini baadaye waliacha kushirikiana nao.

"Watu hawa walikuwa tu  kwa sbabu ya siasa. Walitusahau. Waliacha kuchukua simu zetu mara tu tuliposoma mabaki ya binti yetu," anasema Bi Auma.

Anahusika kikamilifu katika shughuli za kisiasa katika eneo hilo na atakuwa akigombea kwa tikiti ya Chama cha UDA.

Wiki iliyopita, Auma anasemekana kuwa miongoni mwa kundi la wafuasi wa DP Ruto ambao walikamatwa kwa kufanya mkusanyiko wa kisiasa haramu.

Kulingana naye, Gavana Obado akiwa mshirika na DP Ruto hapaswi kumzuia kutekeleza matamanio yake ya kisiasa.