Lupita Nyong'o amwandikia msanii Beyonce ujumbe anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Lupita Nyong'o amlimbikizia sifa Beyonce siku yake maalum
lupita-nyongo1
Lupita Nyong'o lupita-nyongo1
Image: Maktaba

Lupita Nyongo alisherehekea siku ya kuzaliwa ya Beyonce kwa furaha na kumnakilia ujumbe wa sifa.

Katika taarifa yake, Lupita alisema kuwa tabia ya Beyonce ya kuwa wa kipekee inaendelea kuhamasisha watu wengi ulimwenguni.

Kulingana na yeye Beyonce sio aina ya mtu ambaye ataomba msamaha kwa kuwa yeye ni nani na hiyo ndiyo sehemu yake nzuri inayomtia moyo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twotter LUpita alikuwa na haya ya kumlimbikizia Beyonce;

"Kuadhimisha miaka 40 ya @beyonce ni jambo la furaha na njia yake isiyo ya kawaida ambayo inahamasisha harakati ya mwili mkali na wa kike !!!! Heri jema siku yako ya kuazaliwa   malkia wetu aliyechaguliwa," Aliandika Lupita.

Kupitia akaunti yake ya mitandao ya kijamii, Beyonce amekuwa katika mstari wa mbele kujaribu kutafuta njia za kusaidia wanyonge na watu wasiojiweza katika jamii