'Ninalinda nafasi yangu,'Muigizaji Sarah Hassan asema anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Muigizaji Sarah Hassan ni miongoni mwa waigizaji ambao wameigiza katika vipindi kadhaa nchini
  • Sarah aliahamika sana kupitia kwenye kipindi cha Tahidi High kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Citizen
Sarah Hassan
Image: Instagram/Sarah Hassan

Muigizaji Sarah Hassan ni miongoni mwa waigizaji ambao wameigiza katika vipindi kadhaa nchini.

Sarah aliahamika sana kupitia kwenye kipindi cha Tahidi High kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Citizen.

Sio kipindi hicho pekeyake balia anaigiza katika kipindi cha Zora kama Zora na muigizaji mkuu katika kipindi hicho.

Mama huyo wa mtoto mmoja huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa alipakia picha kwenye ukurasa wake wa instagram na kumshukuru Mungu kwa kumpa nguvu ya kufanya bidii katika kazi yake.

Pia Sarah amesema kwamba huwa analinda nafasi yake kwani ndio inamuweka.

"Yup, hiyo ni idadi kubwa ya wakati! Ninapenda vibes na nishati nzuri, kucheka, kucheza, tu kuwa na furaha!

Ninalinda nafasi yangu, ambayo inaniweka mimi, katika ulimwengu ambao unaweza kumfanya mtu ahisi kama hawafanyi kazi

Natumaini unalinda nafasi yako, kuweka nishati yako ya akili kwenye ngazi na natumaini unajua unatosha na unafanya kutosha!

Upendo na mwanga wa watu wazuri na furaha ya kuzaliwa kwa wenzangu," Aliandika Sarah.