'Hatuwezi kuwa nchi ya unafiki,'Mashabiki wamuunga Amira mkono kwa kumtetea Edgar Obare

Muhtasari
  • Mashabiki wamuunga Amira mkono kwa kumtetea Edgar Obare
Image: Studio

Amira mkewe mfanyibiashara Jimal Rohosafi, amekuwa akiwasiliana na mashaiki wake mitandaoni, kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram.

HUku akizungumzia masaibu ambayo yamemkumbuka mwanablogu Edgar Obara alisema kwamba sio jambo nzuri na kwamba hakubaliani nalo.

Edgar amevuma wiki jana baada ya kufichua biashara ya 'Wash Wash', huku akaunti yake ya instagam ikifutwa.

"Nimekuwa juu ya mwisho wa hadithi za Edgar lakini sikubaliana na kile kinachotokea kwake ni haki na sahihi ni sahihi

Hatuwezi kuwa nchi ya unafiki yeye ni TMZ ya Kenya na ninaamini kuwa atakuwa upande wa kulia wa historia."

Mwanablogu Edgar Obare alizua mdahalo Jumamosi wakati aliwauliza wafuasi wake kuomba kwa ajli ya familia yake kwa i ndugu yake alikuwa ametekwa nyara.

Siku ya Jumapili juu ya hadithi zake za Instagram, blogger alitangaza kuwa ndugu yake alipatikana katika eneo la Roysambu huko Nairobi.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;