Kwa nini Wakenya mitandaoni wana chuki?-Lilian Ng'ang'a Auliza

Muhtasari
  • Lilian Nga'ang'a amekuwa akigonga vichwa vya habari baada ya kutangaza kuwa ameachana na gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua
Image: INSTAGRAM// LILIAN NG'ANG'A

Lilian Nga'ang'a amekuwa akigonga vichwa vya habari baada ya kutangaza kuwa ameachana na gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua.

Siku chache baada ya,Lilian na MUtua kutangaza kutengana kwao picha za msanii JUliani na Lilian zilienea sana mitandaoni huku mashabiki wakitoa hisia tofauti.

Siku chache zilizopita, Lilian na Juliani walithibitisha kwamba wawili hao ni wapenzi na ni uamuzi wao.

Ni uthibitisho ambao uliibua hisia mseto  itandaoni, huku msanii JUliani akipokea vitisho kama alivyo dai.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram, Lilian alipakia ujumbe na kushindwa ni vipi wakeya mitandaoni wana chuki.

"Kwanini wakenya kwenye mitandao ya kijamii wana chuki na wanamatusi kwa watu ambao hawawajui, na kuwatakia mabaya kila wakati," Aliuliza Lilian.

Ni ujumbe ambao wengi wa wanamitandao walisema kwamba ulikuwa unawaendea wanamitandao na wenye chuki ambao wana dai kwamba wawili hao wataachana tu.