Niwakute!Pendeni maisha yenu,msishindane na vitu vya mitandao ya kijamii,'Akothee awaonya binti zake

Muhtasari
  • Akothee awaonya binti zake, kwa kuishi kulingana na maisha wanayoona mitandaoni

Kwa kweli wengi wanampenda msanii Akothee kwa ushauri wake kwa wasichana na akina mama na hasa kwa kusema ukweli.

Akothee amebarikiwa na wasichana 3 na amekuwa akiwapa ushauri na kuwashika mkono kila mahali.

Kupitia kwenye ukurasa wake wwa instagram msanii huyo aliwaambia binti zake wanapaswa kupenda maisha yao na kuacha maisha ya mitandao ya kijamii.

Akothee alipakia picha ambayo ilikuwa na ujumbe kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram kuzungumza na Wakenya na binti zake.

Kwa mujibu wa picha ilikuwa na ujumbe unaofuata;

"Kwa ushawishi wa watu wa mitandao ya kijamii unaendelea kuepuka uchangamfu Mtu huingia ulimwengu wa uongo

Kwa upande mmoja tamaa ya kupata vifaa kama vile magari ya anasa yanaweza kuwahamasisha na kwa upande mwingine inaweza kusababisha kuchanganyikiwa na unyogovu."

Akothe aliongeza maelezo chini ya picha ya kuonya binti zake  kamwe kujaribu kujisikia au kushindana na maisha ya watu kwenye mitandao ya ya kijamii.

"Kwa veshalia, rue.baby na  Makadia, kamwe jaribu kushindana au kupenda vitu kwenye mitandao ya  kijamii.

Unachoona sio juu ya ardhi, watu wana haribu maisha yao na madeni. Niwakute mnakosa kutumia kwa Vitu Haiwahusu.

Ninyi ni chini ya miaka ishirini na mitano. Jipeni wakati wa kukua. Acha mitandao ya kijamii peke yake "aliandika Akothee.