Wacha kujificha kwa neno kosa ukipatikana ukidanganya-Nadia Mukami

Muhtasari
  • Soma ujumbe wake Nadia Mukami uliozua mdahalo mitandaoni
nadia-mukami-341
nadia-mukami-341

Huku wakiwa Marekani katika  ziara ya muziki katika majimbo tofauti Nadia Mukami na mpenzi wake Arrow Bowy wamekuwa pamoja  tangu walipojitokeza na kutangaza hadharani mapenzi yao kwa kila mmoja ambayo wanamtandao wanafikiria inaweza kuwa inakabiliwa na shida kwa sasa.

Nadia ameibua mdahalo mitandaoni  baada ya kuchapisha maandishi ya kifiche juu ya mambo ya kudanganya kuwalaumu wote ambao huiita ni makosa.

Ni ujumbe ambao wanamitandao wamedai kwamba kunaweza kuwa shida katika uhusiano wake Nadia na Arrow Bowy.

"Makosa ni ajali Kudanganya na kusema uwongo sio makosa., Ni chaguo za kukusudia. Acha kujificha nyuma ya neno kosa ukikamatwa ukidanganya ... " Aliandika Nadia.

Baada ya wawili hao kufichua uhusiano wao wamekuwa wakipkea kejeli kutoka kwa mashabiki huku baadhi yao wakiwapongeza.

Je kunaweza kuwa na shida kati ya uhusiano wa wawili hao au ni kiki tu, kama vile wasanii wengi hufanya ili kupata wafuasi wengi mitandaoni.