"Hata mimi nilikuwa kila kitu kwake" Aliyekuwa mpenzi wa Rotimi amtahadharisha Vanessa Mdee kuhusu mpenziwe

Muhtasari

•Mtangazaji Kim Oprah kutoka Nigeria  ambaye kwa wakati mmoja alichumbiana na Rotimi amemshauri Mdee asiwe starehe sana naye kwani hana uhakika kuwa atasalia kuwa malkia wake milele.

Image: INSTAGRAM

Baada ya kutoa tangazo la ujauzito wake mapema wiki hii, mwanamuziki  mashuhuri kutoka Bongo Vanessa Mdee ameonywa kuwa asijipige kifua sana kuhusu mpenzi wake mwigizaji Olurotimi Akinosho almaarufu kama Rotimi.

Mtangazaji Kim Oprah kutoka Nigeria  ambaye kwa wakati mmoja alichumbiana na Rotimi amemshauri Mdee asiwe starehe sana naye kwani hana uhakika kuwa atasalia kuwa malkia wake milele.

Kupitia ukurasa wake wa TikTok, Oprah amemweleza Mdee kuwa hata yeye kwa wakati mmoja alikuwa amekalia nafasi ambayo kwa sasa ameichukua na licha ya kuhakikishiwa kuwa yeye ni kila kitu kwake  uhusiano wao haukudumu.

Oprah alitengeneza video ambayo ilionyesha picha mbili tofauti, moja ikionyesha Mdee akiwa pamoja na Rotimi huku nyingine akimuonyesha yeye akiwa pamoja na mwigizaji  wakati walikuwa wanachumbiana.

Kwenye Video hiyo Oprah anaonekana akimnyooshea Mdee kidole huku akisema "Usiwe starehe sana mpenzi, hata mimi nilikuwa kila kitu kwake"

Wanamitandao wengi hata hivyo hawajaridhishwa na kitendo cha Oprah huku wengi wakimwambia akubali hali ilivyo na asonge mbele na maisha yake.

Siku ya Jumatano Mdee na Rotimi walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza hivi karibuni.