'Siwezi enda mahojiano kuulizwa juu ya ndugu yangu,'Bahati afunguka kuhusu uhusiano wake na Mr Seed

Muhtasari
  • Msanii Bahati kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii Mr Seed baada ya wawili hao kukosana miaka chache iliyopita
Msanii Bahati na msanii Mr Seed
Image: Moses Matiba

Msanii Bahati kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii Mr Seed baada ya wawili hao kukosana miaka chache iliyopita.

KUlingana na Bahati  uhusiano wake na Mr Seed hauwezi isha kwa ajili ya mambo ambayo yaliandikwa wala kusemwa kwenye mitandao ya kijamii.

"Niliacha kuenda kwenye mahojiano, baada ya wanablogu kueneza maneno mengi kati yangu na Mr Seed, siwezi enda mahojiano kuulizwa kuhusu ndugu yangu Seed

Lica ya yote ambayo tumefanyiana na Seed hayawezi funika kumbukumbu ambazo nimekuwa nazo nikiwa na Seed," Alisema Bahati.

Pia msanii huyo alifichua kwamba licha ya yote ambayo yalisemwa alikuwa anamtembelea mama Seed, na hajawahi muuliza chochote.

Pia alimsifia na kusema kwamba ni mama bora zaidi duniani.

"Baada ya mambo mengi kuandikwa, nilikuwa namtembelea mama Seed, na ahajawahi niuliza chochote kuhusu uhusiano wangu na Seed

Ni mama bora zaidi ambaye nimewahi kutana naye."

Pia aliwatania Mr Seed na mkewe kwa kuwaambia kwamba wanapaswa kuongeza mtoto mwingine.

"Nimo nataka muoongee mtoto mwingine nangoja, Mr Seed nakupenda sana na nakutakia kila laheri katika albamu yako mpya."

Bahati alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya Mr Seed, halfala ambayo ilihudhuriwa na familia, marafiki,wasanii wenzake miongoni mwa watu wengine.

Mr seed album launch