Betty Bayo awaorodheshea mashabiki wake njia tano za kuishi na furaha

Muhtasari
  • Betty Bayo awaorodheshea mashabiki wake njia tano za kuishi na furaha
Betty Bayo

Wakati huu kila mtu anapambana na hali yake kwa ajili ya jamga la corona, na maisha kuwa ngumu baada ya wengi wao kupoteza kazi.

Ni nadra sana kuwapata watu wengi wakiwa na furaha, hasa wakati huu wa sasa.

Ndio kuna wale wanafuraha ya kipekee na wale hawana furaha kwani wanapitia changamoto tofauti katika maisha yao.

Msanii wa nyimbo za injili Betty Bayo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwapa mashabki wake jinsi ya kuwa na kuishi na furaha maishani.

Betty alifahamika sana baada ya kupeana talaka na aliyekuwa mumewe muhubiri Kanyari.

Kupitia kwenye picha ambazo msanii huyo hupakia kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na mpenzi wake anaonekana kwamba ameendelea na maisha yake ya mapenzi.

Kumbuka sheria tano rahisi za kufurahi: Fungua moyo wako na chuki. Fungua akili yako kutoka kwa wasiwasi

Ishi kwa urahisi. Toa zaidi. Tarajia kidogo. Kumtegemea Mungu na nini ingine ofisini kwangu," Aliandika Betty.

Wanamitandao walionekana kupendezwa na ushauri wake Betty kwani wengi wao walimpongezza kwa ajili ya ushauri wake.