logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Ingekuwa mimi namshtaki amechukua mbegu yangu" David Ng'ang'a atetea askofu mwenzake aliyeshtakiwa kutekeleza mtoto

Askofu huyo amesema kwamba watumishi wa Mungu wanapitia majaribu mengi kutoka kwa wanadada ambao wanaenda kwao wakiwa na nia ya kuwatongoza.

image
na Radio Jambo

Burudani14 September 2021 - 07:36

Muhtasari


•,Ng'ang'a alisema kwamba  Bi Judy Mutave ambaye alimshtaki askofu Muriithi anatumia fursa ile kumhadaa  mtumishi wa Mungu.

•Ng'ang'a ameapa kwamba iwapo ni yeye amekabiliwa na masaibu yale angemshtaki mwanadada kwa kosa la 'kumuibia mbegu'

•Askofu huyo amesema kwamba watumishi wa Mungu wanapitia majaribu mengi kutoka kwa wanadada ambao wanaenda kwao wakiwa na nia ya kuwatongoza

v8FEzbqdLrnganga__1576405445_24852

Askofu mashuhuri David Ng'ang'a wa kanisa la Neno Evangelist Center amemtetea askofu mwenzake David Muriithi aliyeshtakiwa kwa kosa la kutekeleza mtoto ambaye alipata nje ya ndoa 

Alipokuwa anahubiria waumini katika kanisa lake, Ng'ang'a alisema kwamba  Bi Judy Mutave ambaye alimshtaki askofu Muriithi anatumia fursa ile kumhadaa  mtumishi wa Mungu.

Kulingana na Ng'ang'a, mwanamke huyo pia ana hatia ya kumtongoza mtumishi wa Mungu.

Ng'ang'a ameapa kwamba iwapo ni yeye amekabiliwa na masaibu yale angemshtaki mwanadada kwa kosa la 'kumuibia mbegu'

"Kama ni mimi namshtaki kortini, kwamba ameiba mbegu yangu. Kwani mwanadada mwenyewe hawezi shtakiwa, mtu ambaye anavumilia kumvua mtumishi wa Mungu suruali. Hapan! Hiyo kesi mimi siwezi kufanya. Mnaonea tu askofu na huyo ni shetani ambaye alikuja kumshika hata kama walilala na yeye. Kama ni mimi nakushtaki uliiba mbegu yangu" Ng'ang'a alisema.

Askofu huyo amesema kwamba watumishi wa Mungu wanapitia majaribu mengi kutoka kwa wanadada ambao wanaenda kwao wakiwa na nia ya kuwatongoza. Aliwasihi waumini kuombea wahubiri ile waweze kukabiliana na majaribu kama yale.

"Niliona huyo msichana, kweli ni majaribu. Nilikaona juzi kwa redio, kweli kamejitengeneza. Saa ingine muombee wahubiri sana" Ng'ang'a alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved