Mpenzi wangu aliita umati wa watu kunipiga akisema mimi ni mwizi-Mwanamume asimulia

Muhtasari
  • Jamaa asimulia jinsi alichapwa na umati kwa ajili ya mpenzi wake
sad man
sad man

Kuna wale walisema kwamba ukiachwa achika, na ukipendwa pendeka, lakini sio wote ambao wanatilia maanani usemi huu.

Mapenzi yanaweza kufanya mtu afanye mambo ambayo hayastahili, huku baadhi yao wakijitoa uhai.

Nikiwa katika ziara zangu kama kawaida, nilipatana na mwanamume ambaye alinisimulia hadithi yake na yale alipitia akiwe na mapenzi kwa mpenzi wake.

Mambo hayakumwendea vyema kwani alivunjika moyo, baada ya mpenzi wake kumtesa.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa na mpenzi wangu wa mwaka mmoja na nusu, ambaye nilimpenda kuliko vyote duniani, baada ya muda alibadilika

Sababu yangu kuu ya kuchukia mapenzi na kuacha kupenda ni kuwa nilienda kumtembelea mwaka wa 2017 , baada ya kufika kwake sikujua kwamba alikuwa na mwanamume mwingine, aliita umati wa watu na kunichapa huku akidai kwamba nililuwa mwizi

Niliacha hali mahututi, hii ni baada ya mwanamume alikuwa ananifahamu alisema kwamba mimi sio mwizi, nililazwaa hospitali kwa muda wa miezi miwili

Hajawahi kuja kuniangalia naendelea aje wala kunijulia hali, si kumbuki jambo mbaya ambalo nilimfanyia wala kumtendea kwani mapenzi yetu yalikuwa ya kipekee, lakini nadhani ni mimi tu pekee nilikuwa kwenye uhusiano wetu

Natumai Mungu atanipa nguvu ya kuenda na kuamini mwanamke mwingine," Alieleza mwanamume huyo.