logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rick Ross aweka wazi uhusiano wake na Hamisa Mobetto

Wawili hao pia walionekana karibu mwezi au miwili iliyopita huko Dubai

image
na Radio Jambo

Habari15 September 2021 - 05:32

Muhtasari


  • Rick Ross aweka wazi uhusiano wake na Hamisa Mobetto
Screenshot.from.2019.10.17.16.25.49

Mwimbaji wa hip hop wa Marekani Rick Ross hatimaye  ameibuka na kuzungumzia uhusiano wake na Hamisa Mobetto.

Alithibitisha kuwa walikuwamarafiki wa karibu sana, wala hakufafanua ukaribu wa uhusiano wao huku akisema kwamba atamwachia Hamisa afafanue uhusiano wao.

Uvumi wa urafiki wao ulienea sana baada ya rappa huyo, kutoa maoni kenye picha za Hamisa alizokuwa anapakia kwenye ukurasa wake wa instagram, huku mashabiki wakisema kwamba wawili hao ni wapenzi.

Wawili hao pia walionekana karibu mwezi au miwili iliyopita huko Dubai na wanamitandao kudai wanaweza kuwa kwenye likizo.

Katika mahojiano na Lil Ommy, Rapa na mfanyabiashara aliyeshinda Tuzo aliongeza kuwa yuko tayari kumuunga mkono  Mobetto kutimiza ndoto zake zote kwa sababu yeye ni mjasiriamali mzuri.

"Lazima niseme ukweli, kuna uhusiano, ni kiasi gani unataka nitakuambia juu yake?, Nitamwachia yeye… lakini yeye ni mtu mzuri sana, mrembo roho na yeye ni mjasiriamali mkubwa na ninataka kumsaidia kuipeleka katika kiwango kingine kwa sababu anafanya kazi nzuri na ninajivunia.

Kuna mambo mengine kadhaa lakini yote kwa yote nataka kumuona akishinda ”alisema Rick Ross.

Rick Ross pia alisema kuwa ana mpango wa kutembelea Tanzania hivi karibuni.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved