'Siyuko tayari kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi,'Mugizaji Maria akiri

Muhtasari
  • Yasmeen Saiedi maarufu kama Maria Wa Kitaa ametoka waziwazi na kuzungumzia hali ya uhusiano wake

Yasmeen Saiedi maarufu kama Maria Wa Kitaa ametoka waziwazi na kuzungumzia hali ya uhusiano wake.

Akizungumza kwenye chatspot, ambako alikuwa anahojiwa na Nana Owiti na Kush Tracy, Maria alisema kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wowote na yeye hayuko tayari kuwa katika uhusiano wowote kwa sababu ya dini yake na pia anahisi kuwa yeye ni mdogo sana na anataka kuchukua muda wake

"Mimi niko katika hilo, inshallah, siku moja yote yatakuwa vizuri. Ninafanya kazi, na kwa kweli, ninapata pesa, lakini siwezi kusema ni kiasi gani ninachopata."

Maria pia alishiriki kuhusu hali yake ya uhusiano. Kuwa Mwislamu, Maria anasema dini yake hairuhusu yeye kuingia katika uhusiano wa kimapenzi bado.

"Ninahisi kama badomimi ni  mdogo, siko tayari kwa uhusiano. Inachukua mengi na inakuja na vitu vingi," aliongeza.

Pia aliweka wazi kwamba alipokuwa anaigiza katika kipindi cha Maria kwamba sehemu ngumu ilikuwa sekta ya mapenzi na kueleza hisia za kimapenzi bali sehemu ya kulia alisema kwamba haikuwa ngumu kwake.

Sasa ni wazi kuwa muigizaji huyo hana mpenzi, na hayuko tayari kuwa kwenye mapenzi.