Ukiwa kwa giza usiamini kila mwangaza unao uona-King Kaka kwa mashabiki

Muhtasari
  • Wiki chache zilizopita mwanamuziki  King Kaka alifunguka kwa umma juu ya ugonjwa wa ajabu amekuwa akipigana kwa miezi, ukimfanya apoteze kilo 33 kwa miezi mitatu
Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Wiki chache zilizopita mwanamuziki  King Kaka alifunguka kwa umma juu ya ugonjwa wa ajabu amekuwa akipigana kwa miezi, ukimfanya apoteze kilo 33 kwa miezi mitatu.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, King Kaka alifichua kuwa hajakuwa na hisia ya ladha kwa kipindi cha miezi miwili na amekuwa akila matunda na kunywa uji tu.

Kupitia kwenye ukurasa wake a instagram Kaka alimewashuri mashabiki wake kuto amini kila mwangaza wanao uona wakiwa kwenye giza.

"Ukiwa kwenye giza usiamini kila mwangaza unao uona," King Kaka aliandika.

Kaka alisema kuwa hata nguo alizokuwa anavaa hapo awali hazimtoshei kwa sasa kufuatia kupungua kwa ukubwa wa kiuno chake.

" Mashabiki wangu, nimeona ni heri niwaambie haya. Nimekuwa mgonjwa kwa miezi mitatu na siku nane. Nilipimwa vibaya. Nimepoteza kilo 33 kwa wakati huo na tulianza kutembea hospitalini. Nimefanyiwa vipimo vyote na hakuna matokeo. Cha kushangaza ni kuwa sina maumivu yoyote na tunatumai kuwa tutapata suluhu hivi karibuni. Kiuno changu kilikuwa na ukubwa wa 36 na sasa ni 33" King Kaka aliandika.

Hata hivyo alieleza kuwa ana matumaini ya kupata nafuu hivi karibuni.