Eric Omondi atimiza ahadi yake amzawadi msanii Mr Seed na milioni 1

Muhtasari
  • Eric Omondi atimiza ahadi yake amzawadi msanii Mr Seed na milioni 1
Eric Omondi
Image: Hisani

Mchekeshaji Eric Omondi hatimaye ametimiza ahadi yake ya kusaidia mwimbaji wa muziki wa wa injili Mr Seed.

Ijumaa Omondi alimpa Mr Seed milioni moja aliyoahidi wakati wa uzinduzi wa albmu ya msanii huyo.

"Tuliahidi na tumewasilisha! msanii MR Seed  ni msanii wa injili tu aliyebaki nchini Kenya. Lazima awe salama na kuungwa mkono. @Merseedofficial" Alisema Omondi.

Wakati wa uzinduzi, wasanii tofauti waliungana mikono na kumchangia Seed na wengine kuahaidi kwamba watasimama naye.

โ€œNilisema pale kwa launch kwamba Seed is among the best Gospel artiste wenye wamebaki in the whole Country and we have to invest in Mr. Seed. Ilikuwa muhimu tukuje tupatie Mr Seed hii Dooโ€ alizungumza Omondi.

Akizungumza baada ya kupokea fedha, Mr Seed alisema;

"Asante sana Eric ... ni mzuri sana ... Eric Alisema milioni 1 na Ametimiza. Kuna Zile Zilisemwa na Hakuna Hata Moja IMETIMIZWA ... Lakini mwishoni mwa siku ya Wakikam Kunisupport na Nilikawa hivyo unyenyekevu na nashukuru Sana ".

Mshabiki wake walishindwa ni kwanini Omondi alisema kwamba Seed ndiye msanii  wa nyimbo za injili wa kiumeambaye amesalia na kushindwa kwani Ringtone huimba nini.

Hizi hapa hisia zao;

ronny254g: Kwani Ringtone anaimba nini?

carsonfrenzy: Umeamua ringtone sio wa Gospel ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

iamshaolinmonk: where is jimmy? bro ๐Ÿ˜ข

team_mushprince: Kumaanisha guardian angel anaimba secular ama..acha comedy babaaa

josephgitau84: Ati na kwa macho za MUNGU tuko equal, how now?