'Flaqo anatuharibia ndoa,'Kabi Wajesus amtania baada ya mkewe kumezea mchekeshaji huyo

Muhtasari
  • Kabi Wajesus adai Flaqo anaharibu familia yake
  • Kulingana na Kabi kupitia ujumbe alioupakia kwenye ukurasa wake wa instagram ni kwamba anaharibu familia yake
Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Baada ya mchekeshaji Flaqo kurudi mitandaoni, akiwa amejaza baadhi ya mashabiki walikana umbo lake mpya na kusema kwamba ni picha ambayo imechorwa, huku baadhi wakimpongeza na kuogopa kuwa wapenzi wao wanaweza mpenda sana kuwaliko.

Muunda maudhui  Kabi Wajesus ni miongoni mwa watu ambao wanaogopa wake zao wanaweza kumpenda Flaqo na kuwaacha.

Kulingana na Kabi kupitia ujumbe alioupakia kwenye ukurasa wake wa instagram ni kwamba anaharibu familia yake.

Milly pia ni miongoni mwa wanawake ambao walipendezwa na misuli yake Flaqo na hakuogopa kumwambia mume wake.

"Huyu Champez @flaqo411 anatuharibia ndoa nimeendea wife @the_urbanhair_salon akaniambia angalia photos za Flaqo 😡😡😡 sasa nimejaribu workout nahaiwork," Aliandika Kabi.

Pia kuna baadhi ya mashabiki wake ambao walimuonea huruma na kukiri kwamba wamepitia papo hapo, kwani wanawake wao wamekuwa wakitamani na kuwapenda wanaume wenye mwili mnene na misuli.