Watu wengi wameenda shule lakini elimu haijawasaidia-Nyota awasuta wenye tabia ya kuwakejeli watu mitandaoni

Muhtasari
  • Nyota awasuta wenye tabia ya kuwakejeli watu mitandaoni

Msanii kutoka mkoa wa wapi Nyota Ndogo kwa mara nyingine amewaka moto mitandaoni baada ya kuwasuta wanamitandao ambao wanatabia ya kukejeli watu wanapopakia chochote kwenye kurasa zao za mitandao.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo amepakia video , na kusema kwamba anaelewa watu wameenda shule lakini kuna wale elimu yao haijawasaidia.

Nyota amewaambia wenye tabia hiyo, baada ya kutoa maoni ya kukejeli mtu wanapaswa kufikiria.

"Kitu ambacho nimegundua watu kwenye mitandao ya kijamii, unapopakia kitu kwenye ukurasa wako mwenye, nimekuja kugundua watu wameenda shule lakini elimu haijawasaidia

Usikimbilie kutoa maoni yako,kwanza soma na uhakikishe kwamba umeelewa nini haswa kimepakiwa pale

Lakini kwa sababu wana vidole na simu, wanatoa maoni kwa jambo ambalo hawajaelewa umemaanisha nini

Tafadhali kabla hujatoa maoni yako kuhusu chochote elewa," Alisema Nyota.

Pia alizidi na kusema

"Kila siku tunaambiwa hatujasoma na wengi waliosoma hali yetu, watu na viatu."