Msanii wa nyimbo za bongo Flava Rayvanny kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemtambulisha msanii wa kwanza ambaye amemsajili kwenye lebo yake.
Kulingana na Rayvanny, msanii huyo anafahamika kama MacVoice, huku akimkaribisha katika lebo yake alimpa ushauri kwamba anapaswa kutambua Mungu,heshima na bidii katika maisha yake.
Rayvanny pia alisema kwamba Raha ya nyumba ni kuwa na mtoto, na kuwasihi mashabiki wake wamshike mkono msanii huyo.
Mungu alikupa kipaji ili kikusaidie Na kwenye Maisha ni muhimu kuzingatia mambo haya !!!1.MUNGU2.HESHIMA3.BIDIIUtayaona mafanikio ukizingatia hayo zaidi Ni wadau Na wapenzi wamuziki ( mashabiki) kumsapoti kijana wenu ili kesho Na kesho kutwa nae awasaidie wengine!!!! GO GOOOO SON @macvoice_tz mjukuu wa @diamondplatnumz
Raha ya nyumba iwe Na mtoto 😂!!!! Baba Na Mwana @macvoice_tz," Aliasema Rayvanny.
Huku akimjibu Rayvanny, msanii huyo alimuomba Mungu ampe Rayvanny maisha marefu.
"❤️❤️ mungu akupe maisha marefu king 🤴 chui."
Hata hivyo MacVoice sio mgeni katika tasnia ya muziki Tanzania, kwani miaka chache iliyopita alikuwa chini ya usimamizi wa Chege Chigunda. lakini wakaachana.