'Siku hizi una hubiri?'Mashabiki wamuuliza Juliani baada ya kuandika ujumbe wa kitabu cha Warumi

Muhtasari
  • Juliani aibua hisia mseto mitandaoni, baada ya kuzungumzia kitabu cha warumi
Msanii Juliani
Image: Instagram/JUliani

Msanii Juliani kwa muda amekuwa akipokea kejeli kutoka kwa wanamitandao baada ya kutangaza uhusiano wake na aliyekuwa mkewe gavana wa Machakos Alfred Mutua, Lilian Ng'ang'a.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram siku ya Jumanne aiandika ujumbe na kusema kwamba kila mtu atahukumiwa  kulingana na kile anajua na kile hajui.

Alikuwa anazungumzia kitabu cha warumi kifungu cha 2, na kusema kwamba kina pendeza sana.

Wanamitandao wengi wamekuwa wakikejeli msanii huyo na kumwambia kwamba alinyakua mke wa wenyewe.

"Romans 2 ni interesting sana.Kila mtu ata get judged kulingana na kenye unajua na kenye hujui.

Though kwa subsequent chapters, inakua clear, ukiwa under grace ... una a better chance for righteousness juu other ways e.g mboka, hazitoshi mboga."

Ni ujumbe ambao uliibua hisia tofauti kutoka kwa wanamitandao, na hizi hapa hisia zao;

jannykeg: Social media watu wana machungu na maisha yao waah😂 what's wrong with sura. Sisi wote tumeubwa kwa mfano wa Mungu.

learcy.photography: Romans!! One of my fav books!! Ha!! Tell 'm!

ruminarummy01: Sikuizi una hubiri??kkk legend😄

praxx254Pia: Ndovu ni kuu! Hatuku judge Owino.

anne_perer: Nimeamini love is blind😮

christinegmukiri: Juliani kuwa celeb ni hard. Usijali. A wise woman like @ngangalillian would choose you over many men. Watu wajiulize mbona ungeweza kuwa in Bob collymore's(RIP) circle. Na you never have stupid scandals. Ju ukona akili. Lilian is blessed to have you