logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bilionea Grand P avunja kiuno chake akijiburudisha na mpenzi wake mwanasoshalaiti Eudoxie Yao

Kulingana na ripoti mbalimbali,  Grand P anahudumiwa katika hospitali ya Metro nchini Guinea baada ya kulalamikia maumivu kwenye kiuno chake siku chache tu baada yake kuonekana akijiburudisha na mpenzi wake mwenye maumbile makubwa kweli.

image
na Radio Jambo

Makala22 September 2021 - 04:14

Muhtasari


•Kulingana na ripoti mbalimbali,  Grand P anahudumiwa katika hospitali ya Metro nchini Guinea baada ya kulalamikia maumivu kwenye kiuno chake siku chache tu baada yake kuonekana akijiburudisha na mpenzi wake mwenye maumbile makubwa kweli.

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu kama Grand P anaripotiwa kulazwa hospitalini baada ya kuugua kwenye kiuno chake alipokuwa anajiburudisha na mpenzi wake mwanasoshalaiti Eudoxie Yao.

Ripoti mbalimbali zinasema kwamba Grand P anahudumiwa katika hospitali ya Metro nchini Guinea baada ya kulalamikia maumivu kwenye kiuno chake siku chache tu baada yake kuonekana akijiburudisha na mpenzi wake mwenye maumbile makubwa kweli.

Wiki chache zilizopita video na picha zilizoonyesha mwanasoshalaiti Yao akiwa amemkalia Grand P zilienezwa sana mitandaoni.

Kwenye video ambayo Grand P alipakia katika ukurasa wake wa Instagram, wapenzi hao wawili walionekana wakishiriki densi huku Yao akiwa amemkalia mbwenyenye huyo.

Inadaiwa kuwa kipindi hicho cha burudani ndicho kilisababisha maumivu makali kwenye kiuno cha msanii huyo mwenye maumbile ya kipekee hadi akapatwa na matatizo ya kusimama imara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved