'Asante kwa maombi,'King Kaka afichua ameongeza kilo 6

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram rappa King Kaka amewajulisha mashabiki wake hali ya afya yake
Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram rappa King Kaka amewajulisha mashabiki wake hali ya afya yake.

Alisema kuwa anafurahiya maendeleo anayofanya na pia aliwashukuru mashabiki wake kwa kumuombea afya yake.

"Haijalishi ushindi ni mdogo kiasi gani bado ni ushindi tu uliangalia uzito wangu na nimepata kilo 6. Kupotezakilo zote hizo haikuwa utani na sasa kuona faida ni motisha kubwa na baraka. Asante kila mtu ambaye alisali Twendelee ubarikiwe. " Ujumbe wa King Kaka ulisomeka.

King Kaka ameugua kwa miezi mitatu na alikuwa ameelezea kupitia mitandao ya kijamii muda si mrefu kwamba alikuwa amepoteza karibu kilo 30 akiwa mgonjwa.

Ni jambo zuri kwamba anaongeza ukilo zake na afya yake inaonekana kuimarika siku baada ya siku.

" Mashabiki wangu, nimeona ni heri niwaambie haya. Nimekuwa mgonjwa kwa miezi mitatu na siku nane. Nilipimwa vibaya. Nimepoteza kilo 33 kwa wakati huo na tulianza kutembea hospitalini. Nimefanyiwa vipimo vyote na hakuna matokeo. Cha kushangaza ni kuwa sina maumivu yoyote na tunatumai kuwa tutapata suluhu hivi karibuni. Kiuno changu kilikuwa na ukubwa wa 36 na sasa ni 33" King Kaka aliandika.

Kaka aliema kuwa hata nguo alizokuwa anavaa hapo awali azikuwa zinamtosheabaada ya  kupungua kwa ukubwa wa kiuno chake.