"Asante kwa kunizalia binti mrembo" Mwanamuziki Willy Paul amsifia baby mama wake mzungu

Muhtasari

•Mwanamuziki  huyo ambaye anafahamika kwa kujipiga kifua kuhusia na umahiri wake wa kuteka wanadada amedai kwamba aliangukia sana kumpata Mama Sonya.

•Willy Paul amesifia sana urembo wa mwanadada  huyo mwenye asili ya Urusi na kumshukuru kwa kumzalia binti mrembo

Image: WILLY PAUL

Mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za kisasa Wilson Radido almaarufu kama Willy Paul anaonekana kuwa na mapenzi makubwa kwa 'baby mama' wake mzungu Victoria Shcheglova.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 28 anajulikana kuweka mahusiano yake siri na haifahamiki wazi kuhusu hali ya uhusiano ilivyo kati ya wawili  hao kwa sasa.

Hata hivyo, Willy Paul amesifia sana urembo wa mwanadada  huyo mwenye asili ya Urusi na kumshukuru kwa kumzalia binti mrembo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanamuziki  huyo ambaye anafahamika kwa kujipiga kifua kuhusia na umahiri wake wa kuteka wanadada amedai kwamba aliangukia sana kumpata Mama Sonya.

"Mama Sonya wangu na marafiki wake. Hapa niliangukia manze. Jina langu ni mkunaji na ukunaji ndio nafanya vizuri zaidi.. Shukran sana mama Sonya kwa kunipatia binti mrembo" Willy Paul aliandika chini ya picha ya wanadada watatu warembo kweli ambayo alipakia kwenye mtandao wa Instagram

Mapema mwaka huu mwanamuziki huo alifichua hadharani wanawake wawili ambao amepata nao watoto pamoja na wanawe wawili Damian na Sonya.

Hata hivyo, Paul  anaonekana kumpendelea zaidi mama ya mtoto wake mdogo, Sonya Wilson kuliko  mwanamke aliyekuwa mpenzi wake wa zamani na mama ya mtoto wake wa kwanza Damian.

Sio mara ya kwanza kwa Paul kuonekana akimsifia malkia huyo wa Urusi mitandaoni. Mwanamuziki huyo amewahi kupakia picha za mwanadada huyo mara kadhaa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuambatinisha na jumbe tamu, jambo ambalo linaashiria kwamba huenda bado wanachumbiana.