Karibu nyumbani,'Msanii Nyota Ndogo hatimaye akutana na mumewe

Muhtasari
  • Msanii kutoka kwenye mkoa wa pwani Nyota Ndogo,ana furaha baada ya kukutana na mumewe.
nyota ndogo
nyota ndogo

Msanii kutoka kwenye mkoa wa pwani Nyota Ndogo,ana furaha baada ya kukutana na mumewe.

Hii ni baada ya miezi kadhaa, kuwa hawayuko pamoja na hawaongeleshani kwa utani ambao Nyota alifanya siku ya 'Fools day' mwaka huu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Nyota alipakia video akiwa na mumewe, wakiwa kwenye gari moshi, kisha kuandika ujumbe mfupi.

"Sabuni ya moyo wangu. Karibu nyumbani," Aliandika Nyota.

Mashabiki wake waliwatakia maisha marefu pamoja, na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

solida_nasra: Woyoooooooooo hakika kila mwenye kusubil yu pamoja na Mwenyezimungu🤗😍😍🤝

fresiagabriel: Mungu awalinde na kamwe shetani asiingie tena kati yenu

enael_john: Wow!!!!!hatimae furaha yako imerudi

faustineelizabeth: Karuuuuudi ha ha ha usije ukasahau tena mwezi wa nne umtanie

brenda_unyakeki: Amkeniiiiiii amerudiiiii😂😂😂😂😂

msuyatausi1: subra huvuta heri waoooo shemeji karibu nyumbani

romessa_achieng_keith: Am happy to see you two together👏😍