"Wewe ni chanzo cha furaha na baraka kwetu" Milly na Kabi Wajesus waadhimisha siku ya kuzaliwa ya kifungua mimba chao Reign Taji

Muhtasari

•Wanandoa hao wawili ambao walifunga ndoa mwaka wa 2017 wametumia fursa hiyo kuandikia mwanao jumbe maalum na kumtakia baraka tele maishani.

Image: INSTAGRAM// KABI WA JESUS

Ni miaka miwili sasa tangu wanavlogu mashuhuri nchini Peter Kabi na Millicent Wambui wamkaribishe mtoto wao wa kwanza Taji Reign duniani.

Taji ambaye si mgeni mitandaoni alizaliwa mnamo Septemba 30, 2019 jijini Nairobi na ameendelea kuwa kipenzi cha wanamitandao wengi kutokana na umaarufu wa wazazi wao.

Kabi na Milly wamekuwa wakimshirikisha mtoto wao kwenye video na kazi zao mitandaoni na hata wamemfungulia akaunti ya Instagram.

Wanandoa hao wawili ambao walifunga ndoa mwaka wa 2017 wametumia fursa hiyo kuandikia mwanao jumbe maalum na kumtakia baraka tele maishani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Milly alisema kwamba Taji ndiye cha cha furaha na baraka katika familia ya Wajesus na kudai kuwa anajivunia kuitwa mama yake.

"Nakupenda sana @TAJIWAJESUS. Wewe ni chanzo kubwa cha furaha na baraka kwetu. Kwa kweli nimebarikiwa sana kuitwa mama yako. Natangaza neema za Mungu zisizo za kawaida, furaha na amani juu ya maisha yako. Ishi kumtumikia siku zote za maisha yako na uendelee kukua kuwa mtu mwema" Milly aliandika.

Kwa upande wake amesema kwamba anampenda sana mwanawe na  amefurahia kuwa naye katika kila hatua ya maisha yake

"Napeza siku zake akiwa mdogo sana lakini nataka kumuona akiendelea kukua kwa hivyo acha tumsherehekee leo. Kheri za kuzaliwa mwanangu. Baba anakupenda sana" Kabi aliandika.

Mashabiki wa wanavlogu hao walijumuika mitandaoni kutakia mtoto wao heri njema za kuzaliwa.