'Nilikuwa mwaminifu kwake sijawahi mcheza,'Fayvanny azungumzia uhusiano wake na Rayvanny

Muhtasari
  • Fayvanny azungumzia uhusiano wake na Rayvanny
fayvanny
fayvanny

Baby mama wa mstaa wa bongo Rayvanny, Fayvanny kwa mara ya kwanza amezungumzia nini haswa kilifanya watengane na msanii huyo.

Fayvanny alifutilia mbali madai kwamba alimdanganya msanii huyo na kuongeza kwamba alikuwa mwaminifu kwake.

Akiwa kwenye mahojiano, Fayvanny alisema kwamba alishangaa sana baada ya madai kwamba ni yeye alimdanganya msanii huyo.

"Hapana nimekataa, sijawahi mdanganya au mcheza,mtafuteni Rayvanny na mumuulize, wwacha nimseme nilikuwa mwaminifu kwake na sijawahi mcheza

Nimeshangaa sana kuwa watu wanaweza sema jambo hilo au madai kama hayo juu yangu," Aliongea Fayvanny.

Pia alisema kwamba ni mapenzi ya Mungu waliachana, hii ni baada ya kuulizwa sababu ya kutengana na baba wa mtoto wake.

"Ni mapenzi yake Mungu."

Wawili hao wamebarikiwa na mtoto mmoja, lakini Rayvanny amethibitisha kwamba ameshaaendelea na maisha yake baada ya kuachana na mama wa mtoto wake.