'Sijawahi kukutana na baba yangu,'Muigizaji Bridget Shighadi afichua haya kuhusu maisha yake

Muhtasari
  • Muigizaji Bridget Shighadi, kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu maisha yake, na jinsi alivyoanza kazi yake ya uigizaj
  • Akiwa kwenye mahojiano na radiojambo, Shighadi alisema kwamba alianza uigizaji wake miaka miwili iliyopita
Bridget Shighadi
Image: Studio

Muigizaji Bridget Shighadi, kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu maisha yake, na jinsi alivyoanza kazi yake ya uigizaji.

Akiwa kwenye mahojiano na radiojambo, Shighadi alisema kwamba alianza uigizaji wake miaka miwili iliyopita.

Huku akizungumzia maisha yake ya utotoni, alisema kwamba amelelewa na mama pekeyake na kuwa ndiye kitinda mimba kwa familia ya watoto 6.

Kulingana na Shighadi hajawahi muona baba yake wala hamjui, pia aliweka wazi kwamba  mpenzi wake Nick Mutuma hakutaka ajiunge na tasnia ya uigizaji, kwani alikuwa anaona hayuko tayari.

"Hakutaka kamwe nijiunge na tasnia ya uigizaji. Labda kwa sababu ya kujitokeza katika tasnia na ukweli kwamba wakati huo sikuwa na hamu ya uigizaji.

Rafiki wa Nick anayeitwa Tosh Gitonga alinipa jukumu kwenye 'Disconnect' lakini nilikataa jukumu hilo lakini alikuwa mkali na hiyo ndiyo hatua yangu ya kuvunja.

Mwanamke mmoja katika Maisha Magic aliniona na kunielekeza kwa uzalishaji wa Giffy ambao unamilikiwa na Lulu na Rashid

Sijawahi muona baba yangu, wala simjui huwa tu namskia mama akimtaja. "

Pia aliweka wazi kwamba uhusiano ake na muiizaji Nick ni rasmi kwani wamebarikiwa na mtoto pamoja.

"Sina haraka ya harusi kwa maana tunaishi pamoja, hangamoto kubwwa ambayo napitia ni kuwa waatu wengi unihukumu kulingana na uigizaji wangu kwa filamu, hawajui kwama ni filamu tu naigiza," Alisema.