(+VIDEO) SK Macharia azawadiwa gari na mkewe akisherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • SK Macharia azawadiwa na Range Rover na mkewe akisherehekea siku yake ya kuzaliwa

Mkurugenzi mkuu katika kampuni ya Royal Media Services SK Macharia amezawadiwa na gari la aina ya Range Rover na mkewe anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia kwenye video iliyoenea sana mitandao mkewe Purity anaonekana akiwa amemshika mkono kumwelekeza Macharia mahali ambao gari hilo lilikuwa limeegeshwa, huku wakiimba wimbo wa kumtakia heru njema anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Macharia ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wametia bidii na wamekuwa wakitia bidii katika kazi yao na kupata utajiri wao.

Miezi miwili iliyopita  Machari aliweka wazi kwamba adad yake mkubwa aliozwa kwa mwanamume ili apate karo ya shule.

Baadhi ya wakenya walimpongeza mkewe Macharia kwa kuhibitisha kwamba yeye ni mke kamili na kwa kumzawadi mumewe.

Heri njema siku yako ya kuzaliwa Macharia