Yvette Obura afunguka kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake Bahati na mkewe wa sasa Diana Marua

Muhtasari

•Yvette ambaye ni mama ya Mueni Bahati amesema kuwa kwa sasa hakuna ugomvi wowote kati yake na Bahati  na kufichua kuwa huwa wanawasiliana mara kwa mara kwani wanashirikiana katika ulezi wa binti wao.

•Yvette aliapa kuwa hawezi patia Bahati nafasi nyingine maishani kama mpenzi wake na kudai kuwa kwa sasa hana hisia zozote za mapenzi kwake.

Image: INSTAGRAM

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki mashuhuri Kevin Kioko almaarufu kama Bahati na mama ya mtoto wake wa kwanza Bi Yvette Obura amefunguka kuhusu uhusiano kati yao ulivyo kwa sasa.

Yvette ambaye ni mama ya Mueni Bahati amesema kuwa kwa sasa hakuna ugomvi wowote kati yake na Bahati  na kufichua kuwa huwa wanawasiliana mara kwa mara kwani wanashirikiana katika ulezi wa binti wao.

Mwanadada huyo alishirikisha wafuasi wake kwenye mtandao wa Instagram katika kipindi  cha maswali na majibu.

Yvette aliapa kwamba hawezi patia Bahati nafasi nyingine maishani kama mpenzi wake na kudai kuwa kwa sasa hana hisia zozote za mapenzi kwake.

"Siwezi" Yvette alimjibu shabiki mmoja aliyetaka kujua kama anaweza patia uhusiano wake na Bahati nafasi nyingine.

Hata hivyo, Yvette alisema kwamba wanashirikiana vizuri na Bahati katika ulezi wa Mueni na kueleza kuwa huwa anaenda nyumbani kwa mwanamuziki huyo mara kwa mara kupeleka bintiye.

'Huwa naenda kwake kupeleka Mueni na huwa naona watoto wake wengine wawili.. ulezi uko sawa kabisa. Nadhani nyote mwaweza kuona hivyo" Alisema Yvette.

Yvette pia alifichua kwamba Bahati anagharamia karo ya shule ya binti wao.

Mwanadada huyo ambaye ana umbo wa mwili wa kumezewa mate na wengi alifichua kuwa ingawa Bahati ndiye baba wa kifungua mimba chake, hakuwa mpenzi wake wa kwanza maishani.

Alisema kuwa alisonga mbele na maisha yake kawaida kama vile watu wengine tu baada ya kutengana na Bahati zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Yvette alisema kwamba hajawahi kuwa na ugomvi wowote na mke wa Bahati wa sasa, Diana Marua ila hawajawahi kuwa na uhusiano wa kirafiki kamwe.

"Hatukuwa na ugomvi.. Vile tu hatukuwahi kuwa na uhusiano" Yvette alimjibu shabiki mwingine.

Alidai kuwa hajawahi kuwa na kinyongo kuona bintiye akiwa na uhusiano mzuri na Diana Marua