Baadhi ya wasanii mashuhuri nchini ambao wamewahi kuchumbia/kufunga ndoa na wapenzi wazungu

Image: INSTAGRAM

Willy Paul

Mwanamuziki Wilson Radido almaaarufu kama Willy Paul amewahi kuwa kwenye mahusiano na mwanadada kutoka Urusi anayetambulika kama Victoria Shcheglova.

Wawili hao hata wamebarikiwa na binti pamoja. 

Willy Paul alitangaza kuzaliwa kwa binti yao Sonya Wilsovna mwishoni mwa mwaka uliopita.

Hata hivyo, staa huyo mwenye umri wa miaka 28 anajulikana kuweka mahusiano yake siri na haifahamiki wazi kuhusu hali ya uhusiano ilivyo kati ya wawili  hao kwa sasa.

Image: WILLY PAUL

Akothee

Huenda mwanamuziki Esther Akoth almaarufu kama Akothee akawa msanii wa kike nchini ambaye amewahi chumbia na kupata watoto na wanaume wengi ziadi na kutokuwa na haya ya kuweka jambo hilo wazi.

Mama huyo wa watoto watano amewahi kuwa kwenye mahusiano na wanaume wawili wenye asili ya Ulaya na hata kupata watoto nao.

Prince Ojwang na Prince Oyoo ni watoto ambao msanii huyo alipata kutoka kwa mahusiano yake na wazungu wawili, mmoja aliyetambulishwa kama Dominic kutoka Ufaransa na mwingine kutoka Uswizi.

Nyota Ndogo

nyota ndogo
nyota ndogo

Mwanamuziki Mwanaisha Abdalla almaarufu kama Nyota Ndogo amekuwa akiweka hadharani uhusiano wake na mzungu kutoka Netherlands.

Nyota Ndogo na bw Henning Nielsen walijitosa kwenye mahusiano zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Mwaka huu uhusiano kati ya wawili hao umekuwa ukiangaziwa sana kwani kuna wakati ulionekana kuyumba. 

Lenana Kariba

Mwigizaji mashuhuri Lenana Kariba alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Helen mwezi Septemba mwakani.

Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa anaishi Uingereza alivisha mzaliwa huyo wa Netherlans katika visiwa vya Carribean.

Octopizzo

Image: HISANI

Rapa Henry Ohanga almaarufu kama Octopizzo amefunga ndoa na mwanadada mzungu ambaye wamebarikiwa na watoto watatu pamoja; Zara, Tracy na Fredy.

Anita Nderu

Mtangazaji Anita Nderu alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Barrett Raftery  mwezi Septemba mwakani katika hafla iliyohudhuriwa na wanafamilia na marafiki wachache.

Barret ambaye ni mwanamazingira ana asili ya Kihindi.