'Mambo mazuri yanatokea kwa watu wazuri'Mkewe Jimal amshukuru mumewe kwa zawadi ya simu

Muhtasari
  • Siku chache tu zilizopita, Jimal na mkewe Amira walionekana kuwa na wakati wa kujifurahisha pamoja na wavulana wao

Inaonekana kama mfanyabiashara Jimal ameamua kurudi kwa mke wake baada ya kuanguka kwa uhusiano wake  na mke wake wa pili ambaye ni Ray Amber Ray.

Hii inakuja baada Amber Ray na Amira wawili kupggana vita vya ndani, kitu kilichofanya Amber Ray aondoe nyumbani kwake na kuishi katika makazi mapya.

Siku chache tu zilizopita, Jimal na mkewe Amira walionekana kuwa na wakati wa kujifurahisha pamoja na wavulana wao.

Kitu ambacho kilikuwa na maoni ya kurudi pamoja baada ya kuanguka  kwa ndoa yao, ni jambo ambalo liliwafanya baadhi ya wanamitandao na mashabiki wao kufurahia kurudiana kwao.

Amira ni mwenye furaha baada ya mumewe Jimal kumzawadi simu ya aina ya iPhone 13 Pro Max.

Alitangaza habari hizo kwa mashabiki wake ambapo alimshukuru Jimal kwa zawadi hiyo alikiri kwamba yeye amezingatia simu yake mpya.

"Wanasema mambo mazuri yanatokea kwa watu wazuri, Asante Jamal," Aliandika Amira.