Sitarajii mtoto mwingine tena, nimetosheka na watoto wawili-Asema Cate Actress

Muhtasari
  • Wengi walimfahamu kupitia katika kipindi cha Mother-In-Law, na ameendelea kutia bidii katika kazi yake huku akifahamika sana mitandaoni
Kate-Actress-looking-great
Kate-Actress-looking-great

Wengi walimfahamu kupitia katika kipindi cha Mother-In-Law, na ameendelea kutia bidii katika kazi yake huku akifahamika sana mitandaoni.

Akiwa kwenye mahojiano muigizaji Cate amefichua kwamba ametosheka na wanawe wawili, na wala hatawahi zaa tena.

Licha ya kuwa na ujauzito mwema wa mwanawe wa pili, amesema kwamba hatarajii kupata mtoto mwingine.

Cate hakusema wala kufichua sababu ya kusema hayo na wala hakujali kile wanamitandao watasema kuhusu usemi wake.

"Sijaolewa kwa muda mrefu kutoa ushauri kwa wanandoa lakini inafanya kazi basi ni nzuri, ikiwa haifanyi kazi basi sidhani wewe unatakiwa kujiua ukijaribu kuifanya ifanye kazi, namaanisha usiteseke

Sidhani kuwa nina usawa, najaribu tu kufanya kile ninachoweza, lakini ni nzuri kwamba nina mshirika anayeunga mkono. Kwa hivyo sio shida kwa mimi. mimi ni mwadilifu

Nina watoto wawili na nimemaliza,"Alisema Cate.

Wakati wa mahojiano, Kate pia alisema anawekeza sana katika sanaa yake ili kuendelea kuwa muhimu katika tasnia.

"Ninajaribu iwezekanavyo kuwekeza tena mara moja kwa wakati ili niweze kuendelea na mwenendo."