logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Ujauzito unafaa kubebwa miezi 24" Mwanasoshalaiti Vera Sidika adai anafurahia kuwa mjamzito

Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amesema kwamba anafurahia sana kubeba ujauzito huku akidai kuwa angependa kupata mwingine punde baada ya kujifungua kifungua mimba chake.

image
na Radio Jambo

Habari05 October 2021 - 08:10

Muhtasari


•Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amesema kwamba anafurahia sana kubeba ujauzito huku akidai kuwa angependa kupata mwingine punde baada ya kujifungua kifungua mimba chake.

•Mama huyo mtarajiwa amesema kuwa amefurahia sana kubeba ujauzito na kudai kuwa anaweza amua kuwa mjamzito kila mwaka.

•Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31 amedai kuwa mwanamke anafaa kufurahia safari hiyo bila vikwazo vyovyote.

Mwanasoshalaiti Vera Sidika amedai kwamba hana majuto yoyote kwa kukubali kubeba ujauzito wake wa kwanza.

Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amesema kwamba anafurahia sana kubeba ujauzito huku akidai kuwa angependa kupata mwingine punde baada ya kujifungua kifungua mimba chake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amesem kuwa bado hajachoshwa na kipindi cha miezi tisa ambacho amekuwa mjamzito na kudai kuwa angependa ujauzito uwe unachukua kipindi kirefu zaidi.

"Eti watu wamechoshwa na ujauzito wangu na sio wao ambao wamenibebea. Wankunywa panadol wakati mimi ndiye naumwa na kichwa. Mimi sijachoka. Kwa kweli ujauzito unafaakuchukua miezi 24. Miezi tisa ni kidogo sana kwangu" Vera aliandika.

Mama huyo mtarajiwa amesema kuwa amefurahia sana kubeba ujauzito na kudai kuwa anaweza amua kuwa mjamzito kila mwaka.

Vera amewasuta sana wanamitandao ambao wamekuwa wakimwambia kuwa wamechoshwa na ujauzito wake na kuwataka wazoee kumuona katika hali ile.

"Nafurahia kuwa mjamzito. Ndio maana nataka kupata mwingine baada ya binti yangu kuja. Inshallah. Kama unafikiria umechoka, hujaona kitu bado. Naweza amua kuwa mjamzito kila mwaka. Heri uanze kujifunza kukubali ama ufunge macho, ublock, uache kunifuata, unifute. n.k" Vera alisema.

Kulingana na Vera, safari ya ujauzito haifai kuwa ya kuchosha. 

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31 amedai kuwa mwanamke anafaa kufurahia safari hiyo bila vikwazo vyovyote.

"Ujauzito haufai kuwa jambo la kuchosha. Mimi nitajipamba!! Nitavaa vizuri, nijipondoe, nicheke, nicheze densi, nikimbie na nishukuru Mungu kwa kunipa uhai" Alisema Vera.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved