'Akili imeoza,'Mchekeshaji DJ Shiti amshtumu vikali muhubiri James Ng'ang'a

Muhtasari
  • Mchekeshaji DJ Shiti amshtumu vikali muhubiri James Ng'ang'a
dj-shiti-2
dj-shiti-2

Miaka nenda miaka rudi mhubiri mashuhuri nchini James Maina Nga'ng'a ameendelea kushangaza Wakenya na utata mkubwa ambao umezingira taaluma yake.

Mwazilishi huyo wa kanisa la Neno Evangelism Center anajulikana kufanya matendo ya kustaajabisha ama kutoa matamshi tatanishi hadharani bila woga wowote.

Hivi majuzi mhubiri huyo alipokuwa anaendeleza ibada kanisani mwake alitangaza wazi jambo moja ambalo angependa lisifanyike wakati safari yake duniani itafika hatima.

"Hawa wasichana wadogo, mimi hawatashika private yangu nikikufa. Eti njoo uone Ng'ang'a, kumbe alikuwa na d*ck kubwa hivi." Alisema Ng'ang'a.

Hata hivyo ujumbe wake haukupokelewa vyema na mashabiki  kwani baadhi ya watu mashuhuri walimkashifu kwa matamshi yake.

Mmoja wa watu mashuhuri waliomkashifu ni pamoja na muigizaji na mchekeshaji DJ Shitti ambaye alisema kwamba Ng'ang'a anaharibu injili.

Pia alidai kwamba watu wa umri wake hawawezi tamka neno kaa hilo mbele ya watu.

Huu hapa ujumbe wake DJ Shiti;

"Huyu anakwanga Bishop ama Mtu wa porno jamani ??? Rika zake wote hakuna mwenye anajua the word dick but kwa sababu yeye anawatch Oily black booty nyiiingi na nudes imejaa kwa gallery akili imeoza..... Anafaa hatua kaaali sana Ana tarnish the Gospel 😮😮😮😮😮," Alisema Shiti.