Kila mtu ako na pombe!Mchekeshaji JB Masunduku afichua jinsi alitumia milioni 1 kwa siku 11

Muhtasari
  • Mchekeshaji maarufu, JB Masanduku akiwa kwenye mahojiano amefichua jinsi alitumia milioni 1 kwa siku 11
JB Masanduku
Image: Maktaba

Mchekeshaji maarufu, JB Masanduku akiwa kwenye mahojiano amefichua jinsi alitumia milioni 1 kwa siku 11.

JB alifunua kuwa baada ya kupokea pesa hizo, alifurahi na kusafiri kwenda Uganda, Rwanda na Burundi ambako alitumia pesa hizo kwa pombe, wanawake na safari za teksi ghali.

Shilingi 300,000 za Kenya ziliibiwa akiwa mlevi.

Kufikia wakati aliporudi Kenya, alikuwa na shilingi 12 tu na ilibidi apigie familia yakekwa ajili ya msaada.

Kwa bahati nzuri, familia yake haikumhukumu kwa kuwa alikuwa bado mchanga na maisha labda yangempa nafasi ya pili.

"Nilipofika Uganda, nilibadilishana Shilingi 100,000 na nikapata UGX Sh1 milioni. Wakati huo nilikuwa mamilionea nchini Kenya na Uganda, nilikuwa na pesa, kwa hivyo ilibidi nisafiri kwa mtindo. Unajua teksi za uwanja wa ndege wa manjano ni ghali vipi,

Nilimwagiza dereva wa teksi anipeleke kwenye kilabu ghali zaidi mjini, sio bora lakini ghali zaidi,

Nilipofika mahali nilipoenda, nikampa dereva simu yangu mpya - ambayo nilikuwa nimenunua kwa Sh112,000- kama ishara ya shukrani

Yeyote anayekunywa bia, wape chupa 5 zaidi, yeyote anayekunywa divai, wape chupa 2 zaidi, yeyote anayekunywa shot, mpe chupa, nitakulipa Mara baada ya kila mtu kuhudumiwa na baada ya kulipa bili, nilishangaa bado nilikuwa na pesa nyingi kwa njia ya sarafu ya Uganda

Nilikuwa nimezungukwa na idadi kubwa ya wakaazi wa kilabu, na katika mchakato huo mtu aliiba Sh 300,000,"lisimulia Masanduku.

Baada ya hayo yote mchekeshaji huyo alipatwa na msoongo wa mawazo ambapo alianza kunywa pombe, na hata kupoteza fursa ya kuandika na kampuni ya BBC.

https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=D8tc2RJdmIU