Heshimu mwanamke ambaye amefanya bidii kwa ajili ya kazi yake-Zuchu

Muhtasari
  • Msanii Zuchu awasuta watu wenye tabia ya kutowaheshimu wanawake
Zuchu-posing-2
Zuchu-posing-2

Kila mwanamke ambaye anafanya bidii katika kazi yake ili kupata riziki ya kila siku anastahili kuheshimiwa, hii ni kulingana na msanii Zuchu.

Msanii Zuchu kutoka Tanzania alifahamika sana baada ya kujiunga na lebo ya muziki ya WCB, inayomilikiwa na staa wa bongo Diamond Pltnumz.

Bidii yake Zuchu imemuona kupewa kazi na kampuni tofauti nchini Tanzania kwa matangazo ya bidaa zao.

Hata hivyo, inaonekanahajafurahi na baadhi ya kampuni anazofanyia kazi.

Katika moja ya machapisho yake, alielezea masikitiko yake na baadhi ya watu aliowafanyia  kazi.

Kulingana na yeye, yeye hufanya kazi nyingi lakini linapokuja malipo, watu huchukua malipo kubwa.

Aliongeza kuwa hafanyi hayo kwa neema kwa sababu wanakubaliana na hata ishara mkataba kabla ya kitu kingine chochote. Alidai heshima ya jumla pamoja na pesa yake.

"Nimesikitika sana na baadhi ya watu ambao nafanya nao kazi,ifikie muda msanii aheshimiwa kwenye mitandao yake ya kijamii inayotumika kutangazia kitu fulani

Hii sio neema wala  sio msaada tunafanya kazi kazi kwa makubaliano basi ifikie hatua mjifunze kuheshimu wasanii," Aliandi Zuchu.

Kama tunavyojua Zuchu huwa hatafuti kiki kwa mashabiki ili kibao chake kivume, lakini alisema kwamba wnawake wanapaswa kuheshimiwa.

"Na kinachokera zaidi ni kwamba unajua wanajua umefanya kazi kubwa kushikilia bango kwa kiasi kikubwa kuchangia ushawaishi kwenye matumizi ya  kampuni zao

Watu wengi au makampuni wakati mwingine muadharau sana wanawake kwenye upande wa malipo,heshimu mwanamke ambaye ametia bidii kwenye kazi yake 

Nilipeni kile nawadai sio ombi."

Je ujumbe wake Zuchu unaendea kampuni gani, ni WCB au ni gani, ni maswali ambayo wanamitandao wanajiuliza.