'Nafasi ya pili ni yenye thamani zaidi,'Nameless amwambia rappa King Kaka

Muhtasari
  • Nameless amshauri Kaka jinsi nafasi ya pili ni ya muhimu maishani
nameless
nameless

Rappa KIng Kaka ni msanii ambaye atakuwa akiyasimulia yote,baada ya kuwa mgonjwa kwa miezi 3, huku ugonjwa huo ukimwona kupoteza kilo 33.

Baada ya kuugua Kaka aliwafahamisha mashabiki wake kuhusu ugonjwa wake.

Zaidi ya yote msanii huyo alitoa kibao akisimulia aliyoyapitia akiwa mgonjwa, huku akimshukuru mkewe mtangazaji Nana Owiti na mama yake, marafiki na ndugu zake kwa kusimama naye.

Wanamitandao,mashabiki,marafiki, na wasanii wenzake wamekuwa wakimtumia jumbe za kumtakia afueni ya haraka.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram siku ya Jumamosi  alipakia picha akiwa na mwanawe huku akisema kuwa maisha yamempa naffasi ya pili kushuhudia mwanawe akikua.

"Nafasi ya kumuona mwanangu akikua,maisha ya pili," Kaka Aliandika.

Msanii Nameless kupitia katika sekta ya maoni alimjibu Kaka na kumwambia kwamba nafasi ya pili ni ya thamani zaidi.

"nafasi ya pili daima yenye thamani zaidi!" Nameless alisema.

Mshabiki wake walikiri jinsi wamefurahi kumuona ananendelea kupata afueni, na kuwa anatabasamu usoni mwake.