Ni ngumu sana kumuacha mtoto wako na mwanamke au mama wa mtoto wako ata kama mmetengana katika uhusiano wenu.
Aliyekuwa mpenzi wake staa wa bongo Rayvanny, na baby mama wake aiwa kwenye mahojiano amekiri na kusema kwamba wawili hao hawana chuki.
Pia alisema kwamba anampenda sana Rayvanny na mtoto wao ndiye sababu kuu ya wawili hao kuwa pamoja.
Mapema mwaka huu Rayvanny na Fayvanny waliachana, huku mama huyo wa mtoto mmoja akimsuta vikali Rayvanny kwa kuanguka kwa ndoa yao.
"Simchukii. Nampenda sana. Anajua hivyo na sidhani kuwa ananichukia. Ananipenda pia sana coz we are good friends
Hamna njia yoyote ambayo tunaweza kuwa maadui. Lazima tuwe tu good friends maana kuna kitu ambacho kinatuunganisha; mtoto wetu," Alisema Fayvanny.
Je kuna njia yeyote wawili hao wanaweza rudiana, licha ya uvumi kuenea kwamba inaweza kuwa wamerudiana?