Mke wangu ni mjamzito ilhali sina uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito-Mwanamume asimulia

Muhtasari
  • Kulingana na jamaa huyo, mke wake ana ujauzito licha yake kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito
sad man
sad man

Ni maajabu ya musa jinsi wanandoa karne hii ya sasa wanakuwa na mipango ya kando, na hata kuwaletea wenzao watoto ambao sio wao.

Kuna baadhi ya wanandoa baada ya kuingia kwenye ndoa kwa muda mfupi wanaachana kwa sababu moja au nyingi, ila sababu kuu ni mmoja wao kuwa na mpango wa kando.

Nikiwa kwenye ziara zangu, mwanamume mmoja alinismulia shida ambayo anapitia.

Kulingana na jamaa huyo, mke wake ana ujauzito licha yake kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nimekuwa na mke wangu kwa ndoa kwa miaka 3 na nusu sasa, nilienda kupimwa na kuambiwa kwamba sina uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito, haya yalitokea mwaka mmoja baada ya kuwa kwenye ndoa naye

Kwa kweli si kumwambia kwamba sina uwezo, lakini sasa ana ujauzito wa miezi 3, ni jambo ambalo lilinishtua, kwa maana nilimuamini kwa kila kitu, kwa hivyo ana mpango wa kando

Hatuwezi sema ni miujiza, sijui ni mwambie ukweli ili aniambie amekuwa na mpango wake kwa maiaka ngapi

Sijui nifanye aje nataka tu ushauri," Alisimulia

Haya basi habari ndio hiyo ushuri wako kwa jamaa huyu ni upi?