Mwanaharakati Boniface Mwangi hatawania kiti chochote katika uchaguzi ujao-Mkewe afichua

Muhtasari
  • Njeri aliweka wazi kwamba mumewe ana roho nzuri, na zaidi ya yote  anapenda kupigania haki za wakenya
NJeri Mwangi
Image: Studio

Njeri Mwangi mkewe mwanaharakati wa haki za binadamu Boniface Mwangi, akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo alifchua kwamba mumewe hatawania kiti chochote mwaka ujao.

Njeri aliweka wazi kwamba mumewe ana roho nzuri, na zaidi ya yote  anapenda kupigania haki za wakenya.

"Nilipatana na Boniface alipokuwa mpiga picha, alikuwa napenda kuendesha pikipiki, alichukua namba yangu ya simu kutoka kwa jamaa ambaye alikuwa rafiki yangu

Mume wangu ni mu mwenye kupigania haki, ni mara nyingi sana amepigania haki za wakenya, lakini wengi wakikuona unasema ukweli na kupigania haki watakueka mahali ambapo wanataka

Licha ya yote Boniface ana utu na roho nzuri," Njeri Aliongea.

Huku akizungumzia uchaguzi wa mwaka ujao, Njeri alisema kuwa;

"Nina uhakika kwamba Boniface hata wania kiti chochote katika uchaguzi wa mwaka ujao, lakini katika maisha ya usoni anaweza jiunga na siasa."