Tunapaswa kushukuru kwa kila kitu tulichonacho-Akothee asema baada ya shabiki wake kusimulia masaibu yake

Muhtasari
  • Msanii Akothee ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamekuwa wakiwasaidia wanyonge
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

KIla mkenya wa kawaida alipitia magumu ya kila siku baada ya virusi vya corona kutangazwa kama janga nchini.

Asilimia kubwa ya wakenya walipoteza kazi, huku uchumi ukianguka na biashara kurudi na nyuma.

Msanii Akothee ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamekuwa wakiwasaidia wanyonge.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo, alipakia ujumbe wa shabiki aliyesema kwamba ana msongo wa mawazo.

Kulingana na shabiki huyo, ana mtoto ambaye hajaingia shuleni ata baada ya shule ya kufunguliwa.

Huu hapa ujumbe wake;

"Najua hapa si mahali pema pa kupakia ujumbe wangu lakini nahitaji usaidizi,niko na msongo wa mawazo sijui nifanye aje

Nina mtoto wa miaka 5 ambaye hajakuwa shuleni, tangu kufunguliwa kwa shule,naishi kiamuthambi kaunti ya Kirinyaga

 mtu yeyote ambaye yuko katika eneo hilo anisaidia na kazi, nina ujauzito wa miezi 5,nitashukuru, ninakata tamaa," Aliandika shabiki.

Baada ya Akothee kuona ujumbe wa shabiki huyo, aliwashauri mashabiki wake kila mtu anapaswa kushuru kwa chochote ambacho ako nacho.

"🤔🤔 Jane Mumbi hapa ndipo nyumbani ?🙏🙏🙏Tunapaswa kushukuru kwa kila kitu tulicho nacho