'Uliniokota ukaniosha,'Ujumbe wa Eric Omondi kwa Mwalimu Churchill anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Daniel Ndambuki anayefahamika kwa sana kama Mwalimu Churchill, anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo
Eric Omondi na Mwalimu Churchill
Image: INSTAGRAM/Eric Omondi

Daniel Ndambuki anayefahamika kwa sana kama Mwalimu Churchill, anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.

Bila shaka Mwalimu amewakuza wachekeshaji wengi nchini, huku baadhi yao wakifanikiwa maishani.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Eric Omondi,Butita,Mammito, Cartoon Comedian,Otoyo,Chipukeezy,Hamo,Jemutai Miongoni mwa wengine.

Mchekeshaji Eric amemwandikia ujumbe anaposhherehekea siku yake ya kuzaliwa huku akisema kwamba alimuokota na kumuonyesha njia.

Pia alisema kwamba atamshukuru milele,kwani hangekuwa Eric kama sio mwalimu.

Huu hapa ujumbe wake;

"Heri njema siku yako ya kuzaliwa FADHEπŸŽ‚πŸŽ‚πŸŽ‚ hakungekkuwa Eric Omondi bila wewe. Uliniokota pale Athi River Ukaniosha ukanionyesha Njia na nitakushukuru milele Mwalimu.

Wewe ndie ulinijenga. Lakini ile shida uliletea wakenya ni wewe tuta ku blame juu huyu mtoto wako ANASUMBUA NCHI NZIMA Siku nenda Siku Rudi. Happy BIRTHDAY. Wacha nikutafute leo tufanye ile kitu. ALAFU KESHO TUKO PALE QUAVER LOUNGE for BIG LAUGHS @mwalimchurchill,"Aliandika Eric.

Baada ya Mwalimu kuona ujumbe wake Eric alimjibu na kumwambia azidi kuwafurahisha wakenya.

"πŸ˜‚πŸ˜‚ Umesemaaaa I am to blameπŸ˜‚πŸ˜‚ Sawa tu..Ahsante na zidi kufurahisha hao hao wakenya.."Alibu Mwalimu.