Yaishe! achana na DNA lea mtoto,'Akothee amwambia Eric Omondi

Muhtasari
  • Eric alizidi na kusema kwamba alimwambia Jacque wafanye DNA lakini alikataa
  • Huku Akothee akitoa maoni kuhusu vuta ni kuvute ya Eric alimwambia kwamba anapaswa kuachana na DNA na kumlea mwanawe
Esther Akoth

Drama kati ya Jacque Maribe na mchekeshaji Eric Omondi imezidi, kuvutia baadhi ya watu mashuhuri, huku baadhi yao wakimshauri Eric amlee mtoto wake.

Wanamitandao wengi waliwachwa midomo wazi baada ya Eric kusema kwamba walitumia kondomu walipokuwa wakifanya ngono na Jacque.

Eric alizidi na kusema kwamba alimwambia Jacque wafanye DNA lakini alikataa.

Huku Akothee akitoa maoni kuhusu vuta ni kuvute ya Eric alimwambia kwamba anapaswa kuachana na DNA na kumlea mwanawe.

"Je, nyie watu mna wazo la nini kinahusisha kufanya safari zisizo na kikomo kwenye mahakama ya watoto? Je, unajua aina ya wazazi utakaokutana nao kwenye mahakama ya watoto πŸ’ͺ.nyinyi nyote ni watu mashuhuri, mtafedheheka sana ,kupanga laini na wazazi hawana viatu

Eric siku hiyo hautaenda na ulinzi wako πŸ€”πŸ€” kwanza hakimu ataona hiyo range rover akushangae vile walinishangaa na V8 nikifukuzana Na baba ya akina Vesha

Eric wachana Na DNA ,sisi wanawake/mama tunaamua nani baba watoto wetu hata kama Sio wako ,tumekuchagua ,wewe lea tu mtoto ni wetu sote

Sikuhitaji kwenda DNA kwa watoto wangu 3 Vesha Rue na fancy , Wote wanafanana na BABA yao

niamini Hadi leo ,jamaa hata haeliwi watoto wake wanakula nini ,wanaishi vipi . Hawa watoto nimewalea kwa mikono yangu ,wakiita watu wasiowazaa Daddy πŸ€”ERIC UNANISIKIA ? @ericomondi," Akotee aliandika.

Aidha alimshauri Maribe awacha kukimbizana na baba mtoto wake, na kulea mwanawe.

"Jacky wewe pia chukuwa kama mzazi ,mpuuze Eric omondi na kuchukua jukumu la maisha ya mtoto wako ,utakuwa na amani , huyu jamaa atakutoa figo ukose pumzi ya kutafuta kuzungumza nawe kama mama asiye na mwenzi wa watoto 5.

Nilipata amani nilipowacha kukimbizana na baby daddies ,mummy roho yangu ilikuwa inatembea kama mchawi ,usiku silali ,mchana sina nguvu 

Ona Sasa hii mbio inatupeleka DNA Tunasumbua mtoto na vitu visivyo stahili . Mummy yaishe! Yaishe !Yaishe !

Mtoto ashajua babake SUPER STAR .MWISHO WA STORY πŸ’ͺ MTANIKUMBUKA πŸ™πŸ»

Huyu mtoto atakuja kuwa mtu Mkubwa sanaa ,na nyota mtaumia kea kumuumiza mtoto mdogo Na mambo yenu ya hasira za peni mbili.

kujeni ofisini tusuluhishe maneno haya madogo. @ericomondi wewe ni kipenzi changu ,kai nyathi osiepna asayi πŸ™πŸ»

Umekutana na wakili mbaya ambaye hana hisia kwa mtoto au chochote?."