Sababu kwa nini wasanii na watu mashuhuri hapaswi kupakia tofauti zao mitandaoni

Muhtasari
  • Sababu kwa nini wasanii na watu mashuhuri hapaswi kupakia tofauti zao mitandaoni
Image: Hisani

Ndio tumewaona na kushuhudia wengi wao wakipakia kutofautiana kwao na ugomvi wao mitandaoni.

Sio mmoja au wawili bali asilimia kubwa ya atu mashuhuri wamekuwa wakipakia tofauti zao na ata kurushiana vita vya maneno.

Kuna baadhi yao wanapakia ugomvi mitandaoni tu ili kutafuta kiki kutoka kwa mashabiki kwa nia tofauti.

Hivi juzi tumeona mcheshi maarufu Eric Omondi akipakia yale yote yalitendeka kati yake na mama wa mtoto wake Jacque Maribe, miaka saba iliyopita.

Hii ni baada ya Jacque kudai kwamba Eric hajakuwa akiwajibika, kwa mtoto wake.

Sio Eric Tu, wakati huo huo mwanamuziki krg the Don, na mkewe walipakia tofauti zao mitandaoni, huku akitishia kuchukua talaka.

Katika makala haya tutazingatia kwa nini watu mashuhuri na wasanii hapaswi kupakia tofauti zao mitandaoni;

1.Kioo cha jamii

Kwa kweli hao wanafuatwa na wengi na hata kufahamika duniani kote kutokana na kazi yao, kwa hivyo wanapaswa kuwa mfano mwema kwa mashabiki wao.

2.Mfano mwema kwa wengi

Katika kizazi na karne hii ya sasa vijana wengi utawapata wakiwa na gumzo wangependa kuwa nani au msanii yupi endapon atakuwa mkubwa.

Hio ina maana mtu huyo ni mfano mwema kwa wengi, na hapaswi kuwaonyesha upande wao mbaya.

Ndio tunajua hamna mwanadamu ambaye ni kamili, lkini wanapaswa kuwa na mipaka ya mitandao ya kijamii, kila mtu yuko mitandaoni ata watoto wetu.