'Heshimu industry yetu,kutoa shati sio comedy,'Bahati amjibu Eric Omondi

Muhtasari
  • Huku msanii Bahati akijibu madai yake Eric alimuomba aweze kuheshimu sekta ya muziki
Bahati
Image: Hisani

Mcheshi asiyepungukiwa na utata maishani  Eric Omondi kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya JUmapili alitoa wito kwa wanamuziki wa Kenya watie bidii zaidi kazini huku akidai kuwa sekta ya burudani hapa nchini imekufa.

Omondi aliwashinikiza wasanii waamke huku akidai kuwa wengi wao wameisha, wamezembea  na wanachosha.

"Tumekuwa wa kutohitajika, wa kutabirika na wa kuchosha. Tunahitaji kutia bidiii zaidi ili turudishe utukufu uliopotea. Lazima tuwekeze kwa sanaa. Mungu anajua mimi najaribu kadri  niwezavyo" Omondi amesema.

Huku msanii Bahati akijibu madai yake Eric alimuomba aweze kuheshimu sekta ya muziki kwani kutoa shati kwake sio ucheshi.

"Since Huyu Jamaa afungue ile Brothel Yake inaitwa Wife Material amepoteza Akili Sana. You think Kutoa Nguo ni Comedy Sasa??? Young Man Respect Our Industry!!! Sijui Unatembeanga na Bouncers Wakichunga Nini? 

Ukweli ni kuwa ndugu yako Mdogo Fred Omondi anatumia akili, nannitaenda kuhariri upya video yangu ya #Adhiambo kutoka tu sehemu ambayo niliweka ili kukuza kazi yako

La mwisho ni kuwa nipigie simu ili nikupe mawaidha jinsi ya kuwaheshimu wanawakekwa mama kiki ambayo ulitumia kwa mama wa mtoto wako Jacque Maribe sio nzuri baba ambaye hawajibiki hana jukumu la kusomea sekta yetu ya muziki  Infact @EricOmondi Umekua Mtu Bladi Fakin 🖕." Bahati Aliandika.

Wanamitandao wengi ikiwemo wasanii kadhaa kama Jua Cali, Khaligraph, Bien, Femi One na Svara wamejitokeza kukosoa maneno ya Omondi.