'Ulipata mtu,'Wanamitandao wamuuliza Joey Muthengi

Muhtasari
  • Joey Muthengi ni mmoja wa watu mashuhuri ambao wanasherehekewa sana na wanamitandao,kutokana na kazi yake ya urembo wake wa kuvutia
  • Muthengi hajakuwa kwenye runinga zetu kwa muda sasa, huku akionekana kufirahia maisha yake mitandaoni
muthengi 3
muthengi 3

Joey Muthengi ni mmoja wa watu mashuhuri ambao wanasherehekewa sana na wanamitandao,kutokana na kazi yake ya urembo wake wa kuvutia.

Muthengi hajakuwa kwenye runinga zetu kwa muda sasa, huku akionekana kufirahia maisha yake mitandaoni.

Hata hivyo, licha ya umri wake na sura nzuri bado hajaolewa na hata wakati mmoja alisema hana mpango wa kuwa na mwanamume au watoto maishani mwake.

Pia alisema Kwamba ameridhika na kuwa peke yake ilimradi familia yake inampenda.

Wanaume kadhaa wamejaribu kuuteka moyo wake kupitia DM yake lakini anabaki kuwa na msimamo.

Alichapisha video inayoonyesha jinsi shamba lao la mashambani linavyostawi kwa mazao na Chris Kirwa alitoa maoni yake akiuliza kama alipata mtu.

Alijitolea kumuunganisha na mmoja wa mpwa wake kwa sababu kulingana naye Nandi ni kaunti kubwa.

"Ulipata mtu ama nimwambie  mpwa wangu mmoja ateleze DM? Nandi ni kaunti kubwa unayoijua."

Joey alifurahishwa na wali hilo ambapo alijibu na kusema;

"@chriskirwa hili ni swali gumu," Ailijibu JOey.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

thee__kaderee___254: πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Ati wakisii wanasema karibu kisii.....Usikubaliiii

bronze_jeru: Alafu unasikia watu wanasema ukambani kumekauka...huku ni kwao?πŸ˜‚πŸ˜‚

orobatsamuel: Am here uncle@chriskirwa tell her to check her Dm am already in