Tuwaruhusu watoto wakue katika mazingira yaliyojaa upendo-Akothee kwa wazazi

Muhtasari
  • Akothee awasisitizia wazazi kuwalea watoto wao kwenye mazingira yaliyojaa upendo
Esther Akoth

Kwa hakika tunapozungumzia wazazi ambao wwamewalea watoto wao na heshima na kuonyesha mfano mwema mitandaoni msanii Akothee hawezi salia nyuma.

Mama huyo wa watoto 5 kupitia kwnye ukurasa wake wa instagram amewashauri wazazi kuwalea watoto wao katika mazingira yaliyojaa upendo.

Pia Akothee amesimulia jinsi alikuwa napigana na baba wa watoto wake mbele ya watoto wake, alisema haya baada ya kupakia picha ya zamani akiwa na wanawe wawili.

Msanii huyo alisisitiza na kusema kwamba miaka 5 ya kwanza kwa mtoto ni ya muhimu, kwani hujenga tabia yake.

"Miaka 5 ya kwanza ya mtoto ni muhimu sana katika kujenga tabia, ni miaka 5 ya kwanza ambayo itaamua mustakabali wa tabia za watoto wako

Inasikitisha sana kuona wazazi wakiwanyima watoto wao fursa ya kuunganishwa na kujua baba/mama yao ni nani

Kusimulia watoto hadithi zisizo sahihi kuwapa watoto mtazamo mbaya na mbaya kuhusu mzazi wao mwingine.

Ni makosa, ni Mbaya sana. Tuwaruhusu watoto wakue katika mazingira yaliyojaa upendo na kukubalika

Nakumbuka nilipokuwa siwezi kumwelewa baba Oyoo na wazimu wangu, nilikuwa nafanya upasuaji kutoka nje 🤣🤣🤣. Watoto wetu walipata tu kuona vurugu moja na ambayo haikua nzuri

Tangu siku hiyo, kutokubaliana OYOO angekuja na kusimama katikati @oyootheprince : baba! Mama ! Hakuna kupigana, hakuna kubishana kila mtu aondoke kwenye sakafu sasa 🤦🏻🤔. Mungu azilinde familia zako 🙏," Allishauri Akothee.